Nenda kwa yaliyomo

Roderick Nash

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Roderick Nash ni mwanahistoria wa mazingira aliyepata Shahada yake ya Sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Harvard mwaka 1960 na Ph.D. kutoka Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison mwaka 1965[1] Tafiti yake (Misitu na Fikra za Wamarekani) 'Wilderness' and the American Mind' imekuwa Andiko la msingi katika historia ya mazingira, ikichunguza dhana ya (Misitu)'wilderness' na nafasi yake katika fikra za Wamarekani. Baada ya kufundisha ndaki ya Dartmouth, alijiunga na Chuo Kikuu cha California, Santa Barbara, ambako alisaidia kuanzisha programu ya masomo ya mazingira mwaka 1970 baada ya tukio la kumwagika kwa mafuta la Santa Barbara mwaka 1969. Tangu wakati huo, programu hiyo imezalisha maelfu ya wahitimu. Nash anajulikana pia kwa utetezi wa elimu ya mazingira na mapenzi yake katika michezo ya maji yenye mawimbi makali rafting.

Tafiti yake ya Misitu na Fikra za Wamarekani.

[hariri | hariri chanzo]

Kupitia maandiko yake, Nash ameeleza mabadiliko ya mitazamo ya Wamarekani kuhusu asili na wilderness kuanzia enzi za ukoloni hadi wakati wa harakati mbalimbali za kifalsafa kama Transcendentalism, Primitivism, Preservationism, na Conservationism[2] . Anaamini kuwa ili Misitu ibaki salama, inapaswa kusimamiwa kwa makini huku tabia za binadamu zikidhibitiwa. Amewahi kuchapisha vitabu vingi vikubwa katika historia ya uhifadhi na maadili ya mazingira, ikiwa ni pamoja na *The Rights of Nature* na *American Environmentalism.* Kazi zake zimechangia kwa kiasi kikubwa taaluma ya historia ya mazingira na harakati za kulinda mazingira nchini Marekani[3].

  1. "Roderick Frazier Nash | American Academy for Park and Recreation Administration". www.aapra.org (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-09-13. Iliwekwa mnamo 2025-09-04.
  2. Nash, Roderick Frazier (2020-02-14). "Wilderness and the American Mind". doi:10.12987/9780300153507. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)
  3. McDonald, Bryan (2001-06). "Considering the Nature of Wilderness". Organization & Environment. 14 (2): 188–201. doi:10.1177/1086026601142004. ISSN 1086-0266. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)